Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) Taifa Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela, ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM ) Mkoa wa Mbeya katika kikao maalumu kilichofanyika June 4, 2024.
Na Dotto Mwaibale
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
(NEC) Taifa Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela amesema amejipanga kutoa mafunzo kwa
vijana wa chama hicho yenye lengo ya
kuielewa miradi yote ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali chini ya Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan mkoani humo ili waende kuisemea kwa wananchi.
Aidha, Mwaselela amemshukuru Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kumpa fursa ya kwenda nchini China kusomea masuala ya uongozi
ambayo yamemuongezea uelewa wa kuwatumikia wananchi na Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
Mwaselela ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao
cha Wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya Umoja
wa Vijana wa CCM (UVCCM ) Mkoa wa Mbeya alisema Rais Samia amefanya kazi kubwa
ya kuwaletea maendeleo mkoani humo hivyo wanakila sababu ya kumshukuru na ni
muhimu kwa vijana hao kuielewa miradi yote iliyotekelezwa na kuwa na ujasiri wa
kwenda kuisema kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Mwaselela ametoa ahadi kwa
vijana hao ya kuwapatia mafunzo ya itikadi ya kuwalinda viongozi wanapokuwa
katika shughuli zao za kichama na ziara mbalimbali za kawaida na kitaifa ambapo
pia alitoa mafunzo ya matumizi sahihi ya fedha.
Akiongoza kikao hicho Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM
Taifa Mkoa wa Mbeya, Timida Fyandomo alimuomba MNEC Mwaselela kuwaisaidi
kuezeka paa la nyumba ya katibu wa umoja huo ambapo alikubali na kuagiza mara
baada ya kuezekwa na kukamilika kwa ujenzi huo katibu huyo mpaka ifikapo
mwishoni mwa mwaka huu awe amehamia katika nyumba hiyo.
Fyandomo alimshuru MNEC Mwaselela kwa msaada huo
alioutoa kwa UVCCM Mkoa wa Mbeya.


